Takriban watu saba wamefariki katika msururu wa machafuko yanayohusiana na wanajihadi kaskazini mwa Msumbiji, duru za ndani zilisema Jumanne, huku Umoja wa Mataifa ukisema watu 10,000 wamekimbia makazi yao.
Mashambulizi yalitokea katika jimbo lenye utajiri wa gesi la Cabo Delgado, ambapo wanajihadi walianzisha uasi wa umwagaji damu mwaka 2017, na ukalazimu ujumbe wa kijeshi wa kikanda mwaka jana ambao kurejesha hali ya usalama.
Watu wanne walikatwa vichwa katika kijiji cha Natupile, wakaazi waliokimbia eneo hilo kwa hofu waliambia AFP.
“Watu kutoka Natupile walipiga picha, kwa hivyo tunajua ilifanyika,” Antonio Kalimuka aliambia AFP kwa njia ya simu.
“Tayari nimeondoka na familia yangu, lakini bado sijavuna mashamba yangu. Nitalazimika kurudi mara tu kukiwa na salama.”
Watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi Jumatano iliyopita waliwaua wafanyakazi wawili katika mgodi wa grafiti unaomilikiwa na Australia, Triton Minerals, kampuni hiyo ilisema.
Siku iliyofuata, vikosi vya kijeshi vya kanda ya kusini mwa Afrika vilifanya mashambulizi dhidi ya waasi katika msitu wa wilaya ya Macomia kaskazini mwa Pemba, mji mkuu wa mkoa.
“Wakati wa operesheni ya pamoja, magaidi waliuawa na wengine kupata majeraha mabaya,” ujumbe huo ulisema katika taarifa.
Vikosi vya jeshi vilipoteza mtu mmoja na majeruhi sita, iliongeza.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa ulikadiria kuwa watu 10,000 walikimbia makazi yao katika wiki iliyopita.
Idadi ya waliokimbia makazi yao inatofautiana mwezi hadi mwezi, lakini mwezi Mei ilikadiriwa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizikwa 730,000 walikimia makazi yao.
Marekani siku ya Jumanne ilitangaza msaada wa thamani ya dola milioni 29.5 kwa Msumbiji kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani wakati mwanadiplomasia Victoria Nuland alipotembelea nchi hiyo.
“Watu waliokimbia makazi yao walikuwa mashahidi wa mauaji, kukatwa vichwa, ubakaji, nyumba kuchomwa moto, na utekaji nyara, na waliripoti kutekwa nyara kwa wavulana kadhaa,” shirika la misaada la Uingereza Save the Children lilisema katika taarifa.
Zaidi ya asilimia 80 ya waliolazimika kukimbia makazi yao ni wanawake na watoto, iliongeza.