Ademola Lookman wa Nigeria ndiye mchezaji bora wa mwaka 2024 barani Afrika.
Nyota huyo anayechezea klabu ya Atalanta inayoshiriki Seria A nchini Italia amekuwa na msimu wa mafanikio kwa mwaka 2024, hasa baada ya kushinda Kombe la Ligi ya Europa huku pia akiwa ndiye mchezaji bora wa msimu kwenye ligi ya Italia.
Lookman alitupia mabao matatu na kuweza kuisaidia Nigeria kufika hatua ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast, mwanzoni mwa mwaka 2024.
Mnaigeria huyo, pia aliweka kambani magoli mawili katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, wakati Super Eagles wakipepetana na Cameroon, kabla ya nyota huyo wa zamani wa Everton ya Uingereza kufunga bao moja dhidi ya Angola katika hatua ya robo fainali ya AFCON 2024.