Afariki dunia kwa UVIKO 19 baada ya kuachiliwa kutoka gerezani.

Damon Thibodeaux

Mwanamume aliyetumikia kifungo cha miaka 16 gerezani kimakosa, miaka 9 baada ya kuachiliwa aaga dunia kwa UVIKO 19.

Damon Thibodeaux alitumikia kifungo cha miaka 16 gerezani kimakosa kabla ya kikosi cha mawakili kuthibitisha kwamba hakuwa na hatia. Miaka tisa baada ya kuachiliwa kwake kutoka gerezani, amefariki dunia baada ya kuambukizwa UVIKO 19.

Damon alikuwa na umri miaka 47, alihukumiwa kimakosa mwaka 1997, na tangu kuachiliwa kwake mwaka 2012 amekuwa akifanya kazi kama dereva wa lori. Kulingana na kakake Damon, alikuwa amejenga maisha yake upya.

“Hakuwa na kinyongo na mtu yeyote, angestahili kuwa na hasira na dunia, lakini hakuwa na hasira na mtu yeyote. Aliomba na akawasamehe wale waliomfunga kimakosa” David, kake Damon alisema.

Damon alikuwa katika kazi yake ya uderevea kama kawaida, baada ya kupata chanjo yake ya pili ya Moderna ya kukabiliana na UVIKO 19,alipoanza kuhisi dalili za ugonjwa huo, David alisema.Kaka hao wawili walikuwa wakizungumza kila siku, na Damon alimwambia kakake David kuwa alikuwa hajihisi vyema ilikuwa mwanzoni mwa mwezi Agosti.