Search
Close this search box.
Africa

Mabingwa mara saba Misri walipata nafasi ya kujiunga na timu 16 bora katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika siku ya Jumatano kwa kuwalaza majirani zao Sudan 1-0, matokeo ambayo yalipelekea nchi nyingine tano ikiwemo Ivory Coast kujiunga na timu 16 bora.

Nigeria ilimaliza katika Kundi D kwa ushindi wa tatu mtawalia walipoishinda Guinea-Bissau 2-0, na kuwaacha washindi wa pili Misri kumenyana na washindi wa Kundi E katika raundi inayofuata, huku kukiwa na uwezekano wa kumenyana na Wana Ivory Coast.

Bao la kichwa la Mohamed Abdelmonem katika kona dakika 10 kabla ya kipindi cha mapumziko kuliwafanya Mafarao kuwaondoa Sudan kwenye kinyang’anyiro hicho. Ivory Coast, Mali, Gambia, Malawi na Cape Verde zilifuzu kuingia katika kundi la timu 16 bora.

Ushindi wa Misri umeihakikishia Cape Verde na Malawi kufuzu kuwa timu mbili kati ya nne bora zilizo katika nafasi ya tatu.

Ivory Coast wanaongoza Kundi E wakiwa na pointi nne, huku Gambia na Mali wakiwa pia na pointi nne katika kundi F kutoka michezo miwili.

Washindi mara tatu wa zamani Nigeria waliendeleza mchezo wa kuvutia katika kinyang’anyiro hicho kwa kuiondoa Guinea-Bissau kwa mabao mawili katika kipindi cha pili kutoka kwa wachezaji Umar Sadiq na nahodha William Troost-Ekong.

Super Eagles watasalia mjini Garoua kucheza na timu iliyo katika nafasi ya tatu katika hatua ya 16 bora siku ya Jumapili.

Cape Verde itamenyana na Senegal ya Sadio Mane mjini Bafoussam Januari 25, huku Malawi ikikutana na Morocco siku hiyo hiyo mjini Yaounde baada ya kufika hatua ya muondoano kwa mara ya kwanza.

Nafasi tatu zilizosalia zitajulikana Alhamisi baada ya duru ya mwisho ya mechi katika Kundi E na Kundi F.

Algeria lazima waishinde Ivory Coast mjini Douala ili kuepuka kuondolewa mapema baada ya kuambulia pointi moja pekee katika michezo miwili.

Tunisia huenda ikakosa wachezaji 12 akiwemo nahodha Wahbi Khazri katika mechi na viongozi wa Kundi F kwa sababu ya UVIKO-19.

Carthage Eagles, washindi wa 2004, watafuzu kwa hatua ya 16 bora iwapo hawatapata kichapo cha mabao sita au zaidi.

Comments are closed