Search
Close this search box.
Africa

Afisa wa Polisi awaua watu sita ikiwemo mkewe

18

Afisa wa polisi nchini Kenya amemuua kwa kumpiga risasi mke wake na watu wengine watano na kisha kujiua mjini Kabete katika kaunti ya Kiambu.

Inasemekana Konstebo Benson Imbasi alimtaka mkewe kufunga duka lao na kuenda nyumbani ambapo majirani walisikia milio ya risasi ikifyatuliwa asubuhi ya Jumanne.

Konstebo Imbasi alitoka nje na kuwashambulia watu saba, watano kati yao walifariki, mmoja amefariki baada ya kufikishwa katika hospitali kuu ya Kenyatta, mwingine angali katika hali mahututi. Afisa huyo wa polisi kisha alijipiga risasi shingoni na kufariki papo hapo.

Inasemekana kuwa vijana watatu na mwendesha pikipiki katika soko ni miongoni mwa watu waliouawa, mwili wa mwanamke ulipatikana katika eneo la tukio pamoja na silaha ya afisa huyo ikiwa na risasi nne.

Polisi wameanzisha Uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Comments are closed

Related Posts