Afrika kupata ‘sauti yenye nguvu zaidi’ katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara (Kulia) akimkaribisha Kristalina Georgieva (kulia), Mkuu wa IMF, kabla ya mkutano katika ikulu ya rais mjini Abidjan Oktoba 5, 2023. (Picha na Sia KAMBOU / AFP)

Nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zitakuwa na “sauti kali” katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) huku likipata kiti cha tatu katika bodi ya utendaji ya wakopeshaji duniani, mkuu wa IMF Kristalina Georgieva amesema.
Georgieva alitoa habari hizo kabla ya mikutano ya wiki ijayo ya IMF na Benki ya Dunia huko Marrakesh, Morocco, mkutano wa kwanza katika bara hilo tangu 1973.
Bodi ya utendaji ya Shirika la Fedha la Kimataifa, ambayo inaongozwa na mwenyekiti wake, Georgieva, ina jukumu la kuendesha shughuli za kila siku za taasisi hiyo yenye makao yake makuu mjini Washington na kwa sasa ina wakurugenzi 24.
Marekani, ikiwa nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, ina sehemu kubwa zaidi ya kura, ikifuatiwa na mataifa yenye nguvu kiuchumi Japan, China na Ulaya magharibi, mbele ya kanda nyingine na mataifa yanayoendelea.
“Nina habari njema kwa Afrika. Tunaendeleza maandalizi ya kuwa na mwakilishi wa tatu wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika bodi yetu ya utendaji,” Georgieva alisema mjini Abidjan, Ivory Coast, siku ya Alhamisi.
“Hatimaye, itachomaanisha ni sauti yenye nguvu zaidi kwa Afrika,” mkurugenzi mkuu wa IMF aliongeza.

Benki ya Dunia pia imetangaza kuwa itaunda kiti cha tatu cha mataifa ya Afrika katika bodi yake yenyewe, uamuzi utakaofanywa rasmi katika mikutano ya Oktoba 9-15 huko Marrakesh.
IMF na Benki ya Dunia zitashughulikia suala la mageuzi ya kitaasisi nchini Morocco huku zikikabiliwa na wito unaoongezeka wa kushughulikia deni na mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi maskini zaidi.