Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko ambayo yameikumba Afrika Kusini imepanda hadi 440 kufikia Jumapili huku mvua ikipungua ikiruhusu shughuli za uokoaji kushika kasi baada ya moja ya dhoruba mbaya zaidi katika kumbukumbu ya nchi hiyo.
Mvua kubwa iliyonyesha katika eneo la pwani ya kusini-mashariki mwishoni mwa juma lililopita ilisababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi ambayo yalipiga jiji la Durban na maeneo jirani.
Kufikia Jumapili watu 443, wakiwemo wafanyakazi wawili wa polisi wa dharura, walikuwa wamekufa kutokana na mafuriko hayo.
Wanasayansi wanaonya kuwa mafuriko na matukio mengine mabaya ya hali ya hewa yanazidi kuwa na nguvu kadiri dunia inavyozidi kuwa na joto kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Takriban watu wengine 63 bado hawajulikani waliko na wanahofiwa kufariki baada ya mafuriko hayo — ambayo ni makali zaidi kuwahi kuikumba KwaZulu-Natal katika kumbukumbu ya hivi majuzi.
Jiji hilo lenye wakazi milioni 3.5 lilitanda mawingu lakini Shirika la Huduma ya Hali ya Hewa la Afrika Kusini lilisema mvua huenda ingenyesha katikati ya wiki.
Lakini shughuli za uokoaji na misaada ya kibinadamu ziliendelea katika kitovu cha jiji hilo ambalo ni kuvutio cha watalii.
Serikali, makanisa na mashirika ya misaada yalikuwa yakipanga misaada kwa zaidi ya watu 40,000 walioachwa bila makao kutokana na mafuriko hayo.
Serikali imetangaza mara moja randi bilioni moja (dola milioni 68) katika ufadhili wa misaada ya dharura.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Hendrietta Bogopane-Zulu alisema baadhi ya wafanyakazi wa kijamii 340 wametumwa kutoa msaada kwa manusura.
Majeruhi wengi walikuwa kutoka Durban, jiji la bandari na kitovu kikuu cha uchumi.
Sehemu za jiji hazina maji tangu Jumatatu baada ya mafuriko kuharibu miundombinu.
Hospitali nyingi na zaidi ya shule 500 zimeharibiwa.
Nguvu ya mafuriko hayo ilishangaza Afŕika Kusini, nchi iliyoendelea zaidi kiuchumi baŕani Afŕika.
Ingawaje eneo la kusini mashariki limekumbwa na mafuriko hapo awali, uharibifu haujawahi kuwa mbaya kiasi hiki.
Raia wa Afrika Kusini hapo awali wameona majanga kama hayo yakikumba nchi jirani kama vile Msumbiji inayokumbwa na vimbunga mara kwa mara.
Nchi bado inatatizika kurejea maisha ya kawadia baada ya janga la Covid na ghasia mbaya mwaka jana ambazo zilisababisha vifo vya zaidi ya watu 350, wengi wao wakiwa katika eneo la kusini mashariki lililokumbwa na mafuriko.