Aliyekuwa Miss USA Cheslie Kryst amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 30 kufuatia kujirusha kutoka kwa jengo refu mjini Manhattan.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 30, aliishi kwenye ghorofa ya 9 ya jengo hilo inasemekana alifariki dunia kwa kujitoa uhai.Tukio hilo la kusikitisha lilithibitishwa na Idara ya Polisi ya Jiji la New York.
“Mshindi wa shindano la 2019 ambaye pia alikuwa wakili aliruka kutoka kwenye jengo la kifahari alikoishi la Orion la orofa 60 lililoko 350 W. 42nd St. mwendo wa 7:15 asubuhi na alipatikana amekufa kwenye barabarani, gazeti la New York Post iliripoti
Cheslie Kryst, aliandika barua mwaka jana kabla ya siku yake ya kuzaliwa ya umri wa miaka 30 ambapo alijadili mambo magumu anayopambana nayo, ikiwemo wakati, watu waliokuwa wakimkashifu mtandaoni na jinsi alivyofanya kazi nyingi na nzito.
“Kila wakati ninaposema “ninakaribia umri wa miaka 30, nilikuwa naogopa kidogo,” Kryst aliandika katika mahojiano yaliyofanywa na jarida la Allure iliyochapishwa Machi 4 na yenye kichwa “A Pageant Queens Reflects on Turning 30.”
“Jamii haijawahi kuwa mvumilivu na wale wanaozeeka, hasa wanawake,” Kryst, mzaliwa wa Michigan ambaye alishinda taji la Miss USA mwaka wa 2019, aliandika.
“Nilipotimiza umri wa miaka 30 nilihisi wasiwasi kwani ilikuwa kama kukumbushwa kwamba sina wakati tena, kuwa si mrembo tena machoni mwa jamii, ilinikera sana.”
Mahojiano hayo yaliweka wazi hali ya kiakili ya Kryst, mwaka mmoja kabla ya polisi kusema kuwa mrembo huyo ambaye pia alikuwa wakili na ripota wa televisheni na mshindi wa tuzo ya Emmy kuruka kutoka jengo la orofa 60 la Manhattan alikokuwa akiishi.
Mahojiano hayo yalichapishwa wiki chache kabla ya siku yake ya kuzaliwa mnamo Aprili 28, Kryst alitafakari juu ya kuzeeka.
Kryst alielezea jinsi baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, aliendelea kusoma katika Chuo Kikuu cha North Carolina cha Wake Forest na akasema “aliamua kupata digrii ya sheria na MBA kwa wakati mmoja.”
Kryst alisema kuwa tangu aliposhinda taji la Miss USA, “wakati nilipokuwa Miss USA nilikuwa na hamu kubwa ya kufanya kazi yangu na kuwa mkweli.”
Alisema alionekana tofauti na “wasichana wa kawaida wa mashindano ya urembo” ambao “mara nyingi wanastahili kuwa warefu na wembamba, wenye nywele nzuri, na mwenendo wa kuvutia.”
“Siwezi kukuambia ni mara ngapi nimefuta maoni ya watu kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii ambayo yalikuwa na emoji za matapishi na matusi wakisema sikuwa mrembo wa kutosha kuwa Miss USA au kwamba misuli yangu ilikuwa haifai kwa mwanamke na kuwa nilikuwa na mwili wa kiume,” alisema.
Kryst alisema hata alivaa taji lake na kuzunguka nyumbani akijua wazi kuwa atalazimika kulirudisha mwishoni mwa muhula wake kama Miss USA.
“Nilifanya nilichotaka badala ya ilivyotarajiwa,” Kryst aliandika mwishoni mwa mahojiano yake. Sasa, ninaingia umri wa miaka 30 natafuta kuwa mwenye furaha, na kuishi kwa masharti yangu –“ na huo nahisi ndio ushindi wangu mtamu.”
Shirika la Miss Universe pia liliomboleza kifo chake, likitoa taarifa ikimtaja kama “mtu mkarimu na mwema sana.”
Saa chache kabla ya kifo chake, Kryst alichapisha picha yake pamoja na nukuu kwenye mtandao ” natumai hii siku itakuletea pumziko na amani.”