Serikali imesitisha bei za mafuta zilizokuwa zianze kutumika Jumatano Septemba 1, na kuunda timu itakayochunguza sababu za ongezeko la bei ya mafuta.
Akizungumza bungeni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Godfrey Chibulunje amesema kila Jumatano, Ewura hutangaza bei mpya za mafuta.
Chibulunje, amesema kuwa walitoa bei mpya za mafuta iliyokuwa ianze kutumika Septemba 1, lakini kwasababu bei imepanda na itaendelea kupanda, serikali imeamua kusitisha bei hizo mpya na bei za mwezi Agosti zitaendelea kutumika.
Zaidi ya hayo, Chibulunje amesema serikali imeunda timu maalum itakayochunguza kwa kuangalia viashiria ambavyo vinasababisha bei kupanda na kutoa maagizo maalum.
Amesema timu hiyo inajumuisha Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Nishati , Wizara ya Madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) , Ewura pamoja na taasisi nyinginezo.