Bei ya mafuta ya Petroli, Dizeli yashuka Kenya

Bei kuu za petroli, dizeli na mafuta taa zilipungua kwa Ksh.8.18, Ksh.3.54 na Ksh.6.93 kwa lita mtawalia katika taarifa ya ukaguzi wa hivi punde wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) iliyotangazwa Jumatatu.

 

bei mpya zinazoanza kutumika Oktoba 15 hadi Novemba 14, lita moja ya petroli kubwa itagharimu Ksh.180.66 jijini Nairobi huku ile ya dizeli ikiuzwa kwa Ksh.168.06.

 

Wakati huo huo mafuta ya taa yatagharimu Ksh.151.39 lita katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

 

“Wastani wa gharama ya petroli iliyoagizwa kutoka nje ya ilipungua kwa asilimia 8.59 kutoka dola za Marekani 697.62 kwa kila mita ya ujazo mwezi Agosti 2024 hadi dola za Marekani 637.70 kwa kila mita ya ujazo Septemba 2024; dizeli ilipungua kwa asilimia 5.52 kutoka dola za Kimarekani 673.36 kwa kila mita ya ujazo hadi dola 636.22 kwa kila mita ya ujazo ,” Mkurugenzi Mkuu wa EPRA Daniel Bargoria amesema.

 

Mafuta ya taa yamepungua kwa asilimia 6.73 kutoka Dola za Kimarekani 668.34 kwa kila mita ya ujazo hadi Dola 623.39 kwa kila mita ya ujazo.