Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Benin yawaachilia wafuasi 30 wa upinzani wakati wa ziara ya Macron - Mwanzo TV

Benin yawaachilia wafuasi 30 wa upinzani wakati wa ziara ya Macron

Rais wa Benin Patrice Talon akimkaribisha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika ikulu ya Marina huko Cotonou Julai 27, 2022, wakati wa ziara rasmi ya Macron nchini Benin.. (Photo by Ludovic MARIN / AFP)

Benin imewaachia huru wafuasi 30 wa upinzani waliokamatwa wakati wa uchaguzi wa 2021 ambapo Rais Patrice Talon alishinda muhula wa pili, chanzo kikuu cha mahakama kilisema Jumatano.

Uamuzi huo ulikuja wakati wa ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye alikutana na Talon katika mji mkuu wa Cotonou.

Taifa hilo la Afrika Magharibi lilisifiwa kwa muda mrefu kwa demokrasia ya vyama vingi, lakini wakosoaji wanasema uhuru umemomonyoka chini ya Talon mwenye umri wa miaka 64 aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2016. Mahakama maalum ya uhalifu wa kiuchumi na ugaidi, inayojulikana kama Criet, iliwaachilia watu 30 waliokamatwa wakati wa uchaguzi, na kuwaweka chini ya usimamizi wa muda wa mahakama, chanzo kilisema.

Miongoni mwa walioachiliwa ni viongozi na wanaharakati wa vijana wa chama cha upinzani cha Democrats.

Tangazo hilo lilikuja saa chache baada ya Talon kutupilia mbali ukosoaji wa serikali yake kuwa inawashikilia wafungwa wa kisiasa baada ya kufungwa jela mwaka jana kwa viongozi wawili wakuu wa upinzani.

Nchi hiyo ndogo ya Afrika Magharibi iliuyoko kati ya Nigeria na Togo ilikuwa inajulikana kwa kustawi kwa demokrasia ya vyama vingi, lakini wakosoaji wanasema Talon imeiongoza nchi hiyo kwa njia ya kimabavu.

Talon alikuwa akizungumza wakati wa ziara ya siku moja ya Macron huko Cotonou baada ya kusafiri kwenda Cameroon.

“Nchini Benin, hakuna wafungwa wa kisiasa, hakuna mtu anayezuiliwa Benin kwa maoni yake ya kisiasa,” Talon alisema, akijibu maswali ya waandishi wa habari huku Macron akiwa upande wake.

“Lakini watu wanazuiliwa kwa kufanya makosa na uhalifu katika uwanja wa kisiasa, hiyo ni kweli.”

Macron hakuzungumza kuhusu hali ya kisiasa nchini Benin wakati wa hotuba yake.

Talon alisema inawezekana kwamba msamaha unaweza kutolewa kwa viongozi wa upinzani waliozuiliwa, alipoulizwa kuhusu kuwaachilia viongozi hao wawili.

“Tunapaswa kuwa na uwezo wa kurekebisha hali ya kisiasa ili kutoa picha nzuri, inayofaa kwa maendeleo ya kiuchumi,” Talon alisema.

“Taswira ya nchi yetu imechafuliwa kidogo na hali ya kisiasa ambayo Benin imepitia hivi majuzi. Sioni aibu kwa hilo.”

Kiongozi wa upinzani nchini Benin Reckya Madougou alihukumiwa mwezi Disemba kifungo cha miaka 20 jela kwa ugaidi na mahakama maalum katika mji mkuu wa Porto-Novo baada ya kesi fupi ambayo mawakili wake walilaani kama ‘shambulio la kisiasa.’

Madougou alikuwa mmoja wa viongozi kadhaa wa upinzani wa Benin waliopigwa marufuku kugombea katika uchaguzi wa mwaka jana mwezi Aprili ambapo Talon alishinda muhula wa pili kwa asilimia 86 ya kura.

Waziri wa zamani wa sheria, alikamatwa huko Cotonou mwezi Machi — wiki chache kabla ya uchaguzi — akishutumiwa kwa kufadhili operesheni ya kuua wanasiasa ili kuzuia upigaji kura na kujaribu ‘kuyumbisha’ nchi.

Kiongozi mwingine wa upinzani Joel Aivo, profesa ambaye alikuwa amezuiliwa kwa muda wa miezi minane, pia alipatikana na hatia mwaka jana ya kupanga njama dhidi ya serikali na utakatishaji fedha.

Wote wawili walihukumiwa na mahakama maalum inayoshughulikia ugaidi na uhalifu wa kiuchumi.

Wakosoaji wanasema mahakama hiyo, iliyoundwa na serikali ya Talon mwaka 2016, imetumiwa kuwakandamiza wapinzani wake.