Search
Close this search box.
Europe

Bibi arusi, mpishi wakamatwa kwa kutia bangi kwenye chakula cha harusi

20

Bibi arusi kutoka Florida nchini Amerika na mpishi wake wamekamatwa baada ya kufanya mizaha ambayo inadaiwa waliweka bangi kwenye chakula kilichotolewa kwenye harusi yake iliyofanyika mwezi Februari, vyombo vya habari viliripoti.

Kulingana na hati za korti, mamlaka walifika katika ukumbi wa harusi ya Andrew Svoboda na Danya Svoboda baada ya wageni wao kadhaa kuitisha huduma za dharura baada ya kujihisi wagonjwa.

Douglas Postma, mjomba wa bwana harusi, aliwaambia wahudumu wa afya kwamba alihisi moyo wake ukienda kasi na alianza kuwa na mawazo ya ajabu baada ya kula saladi, pasta na mkate.

Ushuhuda huo ulikuwa sawa na ule wa wageni wengine katika sherehe hiyo, iliyofanyika katika jiji la Longwood, kaskazini mwa Orlando.

Mke wa Postma alijisikia vibaya zaidi na ikabidi alazwe katika hospitali ambapo THC, kiungo kikuu cha bangi inayoathiri akili, ilipatikana kwenye damu yake.

Miranda Cady, rafiki wa bibi harusi, alihisi ‘kama moyo wake ungesimama’ baada ya kula mkate na mafuta.

Alimuuliza mpishi, Joycelin Montrinice Bryant, ikiwa alikuwa ameweka bangi kwenye chakula.

Mpishi akasema ndio.

Bibi harusi pia alithibitisha kuwa chakula hicho kilikuwa kimejaa bangi, akionekana kufurahishwa na utani wake, kulingana na taarifa ya Cady kwa mamlaka.

Wenye mamlaka walichukua sampuli za vyakula na vyombo vya glasi, na uchunguzi wao ulithibitisha kuwa chakula kilikuwa kimetiwa bangi.

Wawili hao wameshtakiwa kwa kukiuka sheria za serikali dhidi ya uandaaji wa chakula na bangi pamoja na uzembe.

Wote wawili wameachilia kwa dhamana na watafikishwa mbele ya hakimu mwezi Juni.

Comments are closed

Related Posts