Biden atia saini agizo kuu la kutunga mageuzi katika idara ya polisi kwenye kumbukumbu ya mwaka wa pili wa kifo cha George Floyd

WASHINGTON, DC -MEI 25: Akiwa na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, wabunge na wajumbe wa baraza la mawaziri, Rais wa Marekani Joe Biden atia saini agizo kuu la kutunga mageuzi zaidi ya polisi katika Chumba cha Mashariki cha Ikulu ya White House mnamo Mei 25, 2022 huko Washington, DC. MAY Anna Moneymaker/Getty Images/AFP (Photo by Anna Moneymaker / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via AFP)

Rais Joe Biden ataadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa pili wa mauaji ya George Floyd siku ya Jumatano, siku moja baada ya shambulio la risasi shuleni Robb Elementary mjini Uvalde jimbo la Texas.

Ilikuwa sherehe ya kuashiria maridhiano, kati ya familia za waathiriwa wa ukatili wa polisi pamoja na wawakilishi wa idara ya polisi.

Lakini mauaji ya shule huko Uvale, Texas, ambapo watoto wa shule 19 na walimu wawili walikufa, yatakuwa akilini mwa kila mtu Biden atakapotia saini amri iliyoelezewa kuwa ya kihistoria ya utawala wake, inayolenga kukuza uwajibikaji na kuimarisha viwango vya uwajibikaji katika kitengo cha polisi.

Utiwaji wa saini unakuja miaka miwili baada ya kifo cha Floyd huko Minneapolis, ambacho kilizusha maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi ambao ulienea kote Amerika na duniani kote kwa ujumla.

Floyd, Mmarekani mwenye asili ya Afrika, aliuawa na afisa wa polisi aliyepiga magoti shingoni mwake kwa takriban dakika 10 wakati alipokuwa akimkabili.

“Ili kupata uponyaji wa kitaifa, lazima tukubali kwamba ukatili wa polisi umeathiri zaidi watu weusi,” Ikulu ya White ilisema.

Sheria hiyo, ambayo imechukua muda wa miezi kufanyiwa kazi, inatoa mfululizo wa hatua ambazo zitahusu mashirika ya kutekeleza sheria nchini humo.

Amri ya utendaji inaanzisha hifadhidata ya kitaifa ya utovu wa nidhamu wa polisi, inaamuru matumizi ya kamera zilizovaliwa mwilini na kupiga marufuku baadhi ya matumizi ya kubana mtu koo anapokabiliwa na polisi.

Lakini vikwazo hivi havitawekwa kwa majimbo na mamlaka za mitaa, ambazo nchini Marekani zina mamlaka makubwa sana ya polisi na mahakama.

Kwa hilo, itachukua sheria, iliyopitishwa na Congress, ambayo rais ameshindwa kupitisha.

Biden hajaweza kuimarisha sheria za bunduki, kutoka kupiga marufuku umiliki wa bunduki hadi kuamuru afya ya akili na ukaguzi wa historia ya uhalifu kwa wateja wa bunduki wakati wa kununua silaha.

Kama ilivyo kwa mageuzi ya polisi, utawala umeshindwa katika juhudi zake za kuweka sheria kali, kwa mfano kuongeza vikwazo kwa kile kinachoitwa ‘bunduki fiche.’

Maadhimisho ya kifo cha Floyd, mauaji katika shule ya Texas na pia, siku kumi zilizopita, mauaji ya kibaguzi huko Buffalo, yote ni ukumbusho wa kikatili wa kushindwa kwa Biden kutimiza ahadi zake za kupunguza mashambulio ya bunduki.

Lakini Chama cha Democrats kina idadi ndogo tu ya wabunge katika Bunge la Congress kwa hiyo kushindwa kuleta mabadiliko makubwa.

Na kwa kuongezea, Biden anakabiliwa na Mahakama ya Juu ambayo mtangulizi wake Donald Trump ametoa msimamo thabiti wa kihafidhina.

Kuongeza kwa haya yote haiba ya Biden mwenye umri wa miaka 79, mtetezi mkuu ambaye angependa kutawala kwa makubaliano, ambayo katika Amerika ya leo inaonekana kuwa haiwezekani.

Tangu Amerika ilipokumbwa na ongezeko la watu waliopigwa risasi tangu mwanzoni mwa mwaka huu, rais bado hajafanikiwa kumteua mkurugenzi wa Ofisi ya Pombe, Tumbaku, Silaha za Moto na Vilipuzi.

Shirika hilo kwa hakika halijapata kiongozi wa kudumu tangu 2015.

Jaribio la kwanza la uteuzi lililofanywa na Ikulu ya White House, ikiwa na mfuasi mkali wa udhibiti kama mgombea wake, liliondolewa baada ya mzozo mkali.

Biden amezindua mgombea mpya, Steve Dettelbach, mwendesha mashtaka wa zamani ambaye anaanza mchakato wa kusikilizwa kwa Seneti wiki hii, ambapo kuna uwezekano akakabiliwa na upinzani wa Republican.