Bingwa wa dunia Mary Moraa ashinda taji la Diamond League katika mbio za mita 800,Doha

Katika nafasi ya pili, bingwa huyo aliweza kufuatiwa kwa karibu na Muingereza Jemma Reekie (1:58.42), Benin Noelie Yarigo wa uingereza (1:58.70) katika nafasi ya tatu, Muethiopia Habitam Alemu (1:59.08) katika nafasi ya nne na bingwa wa dunia mwaka 2019 Halimah Nakaayi kutoka Uganda (1:59.48) akatwaa nafasi ya tano, mtawalia. Mbio hizo ziliwahusisha wanariadha 11.

Taji hilo la Dora linajiri katika ziara yake ya kwanza nchini Qatar. Na kwa sasa Moraa anapanga kushiriki tena katika mbio za 600m katika mashindano ya USAF Los Angeles Grand Prix mnamo Mei 9, 2024 nchini Amerika ambako anapanga kuvunja rekodi nyingine.

Baadaye, Mei 25, 2024 anatarajiwa kushiriki katika mbio za 800m katika mashindano ya Eugune Diamond League, itakayofanyika nchini Amerika.

Kando na Moraa kutoka nchini Kenya, bingwa wa dunia wa kurusha mkuki, 2015, Julius Yego, mfalme wa mbio za 1500m, 2019 Timothy Cheruiyot, bingwa wa dunia na Afrika wa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 wa umbali huo Reynold Cheruiyot, Abel Kipsang pamoja na Brian Komen, walishiriki katika mashindano hayo ya Dora.