Boniface Mwangi aachiliwa kwa Dhamana ya Ksh milioni moja

Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi Amefikishwa Mahakama ya Kahawa kwa Mashtaka ya Umiliki Haramu wa Risasi Butu na Mabomu tatu ya Machozi (teargas).

Boni, kama anavyofahamika alifikishwa mbele ya Jaji Gideon Kiage ambapo alikana mashtaka yote mawili na kuachiliwa kwa Dhamana ya Shilingi Milioni Moja (Zaidi ya Milioni 20 za Tanzania)

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, anadaiwa kupatikana na vifaa hivyo vya kijeshi kinyume cha sheria.

Awali Boniface Mwangi alikuwa akizuiliwa kwa kosa la ugaidi lakini kiongozi wa mashtaka akamwondolea Mwangi Mashtaka hayo. Alikamatwa siku ya jumamosi jioni nyumbani kwake Lukenya, Kaunti ya Machakos na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Pangani jijini Nairobi.

Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena tarehe 19 Agosti 2025.