Bunge la Tanzania lilimchagua spika mpya siku ya Jumanne kufuatia kujiuzulu kwa mtangulizi wake katika mabishano ya hadharani na rais yaliyotikisa chama tawala.
Tulia Ackson, ambaye amekuwa naibu spika tangu 2015, aliwashinda wagombea wengine wanane wa upinzani.
“Naamini tumemchagua mtu sahihi ambaye ataliongoza bunge katika mwelekeo sahihi,” alisema mbunge mwandamizi William Lukuvi aliyesimamia uchaguzi huo.
“Anajua mipaka yake kama spika na anajua kuna mkuu wa nchi ambaye ni Samia Suluhu Hassan.”
Ackson mwenye umri wa miaka 46 anachukua nafasi hiyo wakati ambapo kumeibuka mipasuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati kikijiandaa na uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025.
Samia Suluhu Samia Hassan amewatuhumu wapinzani wake kwa kutaka kuharibu uongozi wake tangu awe kiongozi wa Tanzania.
Samia Suluhu ni Rais wa kwanza mwanamke nchini humo na alikuja uongozini mwezi Machi mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla chake Rais John Magufuli.
Mtangulizi wa Ackson, Job Ndugai alijiuzulu mwezi uliopita baada ya kumkosoa Hassan kutokana na kile alichokiita Tanzania kukopa kutoka nje ya nchi na kuishutumu serikali kwa kuzunguka na “bakuli la omba omba.”
Matamshi hayo yalizua mjadala kuhusu viwango vya madeni ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambavyo vilifikia karibu dola bilioni 28 mwezi Novemba, kulingana na takwimu zilizochapishwa na benki kuu ya Tanzania.
Hassan mwezi uliopita alilifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri na kuwafuta kazi wajumbe kadhaa wakuu wakiwemo mawaziri wa sheria, nyumba, viwanda na uwekezaji.
Ametaka kuvunja baadhi ya sera za Magufuli, lakini ametajwa kuwa “dikteta” na upinzani, na hofu imesalia kuhusu hali ya uhuru wa kisiasa na vyombo vya habari.