Mlipuko katika mgodi wa dhahabu huko Burkina Faso Jumatatu alasiri uliua takriban watu 55 na kujeruhi idadi saw ana hiyo, vyanzo vya ndani na vya matibabu vilisema.
Mlipuko huo, katika eneo la muda la kuchimba dhahabu huko Gomgombiro kusini-magharibi mwa nchi hiyo ulitokea wakati hifadhi ya baruti ilipolipuka, walisema maafisa wa eneo hilo na wafanyikazi wa hospitali.
Idadi ya waliofariki ni 50, afisa wa eneo hilo ambaye alitembelea eneo hilo aliema.
Lakini chanzo cha habari cha hospitali kilisema: “Takriban majeruhi watano wamefariki dunia kutokana na majeraha, na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 55,”na kuongeza kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka kwani baadhi ya waliojeruhiwa walikuwa katika hali mbaya.
Wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa watu 60 au zaidi waliojeruhiwa katika mlipuko huo, wengi wao wakiwa katika hali mbaya, chanzo kiliiambia AFP.
Mkazi wa Gomgombiro alisema mlipuko huo umesababishwa na moto katika eneo ambalo baruti za magendo zilikuwa zikihifadhiwa, na ambalo pia lilikuwa soko la mgodi huo.
Mkazi huyo alielezea matukio ya kutisha kutoka eneo la mlipuko huo, ambao uliacha shimo kubwa na miti kung’olewa.
Antoine Marie Sylvanus Doamba, kamishna mkuu wa jimbo la Poni, alisema baada ya kutembelea eneo la mlipuko kwamba wakati idadi ya awali ya miili ilikuwa 48, imeongezeka hadi 55.