Zaidi ya watu milioni 5 wakimbia vita nchini Ukraine
Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi amesema waukraine 5,034,439 wameondoka nchini mwao tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi tarehe 24 ya mwezi Februari mwaka huu.