Kanda ya CCTV iliyotolewa na mwendesha mashtaka Jumanne inaonyesha Irvo Otieno akibanwa sakafuni na maafisa wengi wa usalama katika kituo cha afya ya watu waliyo na matatizo ya akili katika jimbo la Virginia katika muda mfupi kabla ya kifo chake mapema mwezi huu.
Ofisi ya Mwanasheria wa Jumuiya ya Madola ya Jimbo la Dinwiddie Ann Cabell Baskervill pia ilitoa mawasiliano kuhusu tukio hilo ambapo mpiga simu aliomba kuletwa kwa ambulenzi akisema otieno hakuwa anapumua.
Simu hiyo ya dharura na kanda ya video kwa ujumla yalielezea kwa kina matukio yaliyojiri na kusababisha kifo cha otieno mwenye umri wa miaka 28 na mwenye asili ya kiafrika (kenya). Kwa mjibu wa baskervill, Otieno alifariki tarehe 6 machi mwaka huu alipokuwa akihamishwa kutoka jela ya Kaunti ya Henrico hadi Hospitali ya central State
Kutokana na kisa hiyo maafisa saba wa polisi na wauguzi watatu wa hospitali hiyo wamefunguliwa mastaka ya mauaji.
Kisa hicho kimewakosesha Familia ya otieno usingizi na sasa inaomba haki kutendeka na wahusika kuadhibiwa vikali kwa mujibu wa sheria.
‘’Mwanangu aliachukuliwa kama umbwa, hata vibaya sana kuliko mbaya. Hii niliona ka macho yango mimi mwenyewe’’ alisema mamake otieno
Otieno alikamatwa na maafisa wapolisi marekani kutokana amri ya dharura kwa kuwa ana ugojwa wa akili jambo lililokuwa likimfanya kuwa na fujo wakati mwingine. Otieno aliondoka kenya akiwa na umri wa miaka nne kulekea marekani ambapo amekuwa akiishi na familia yake