Maandamano ya Chadema inazidi kuchacha moto nchini Tanzanaia.Tayari maeneo kadha yameshuhudia idadi kubwa ya waandamanaji ikiwemo Mbeya na Dar es Saalam. Maandamano hayo yaliitishwa na chama kikuu cha upinzani kikiongozwa na mwenyekiti wake Freman Mbowe.
Maandamano yanalenga kuishinikiza Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau mbalimbali kuhusu masuala ya uchaguzi.
Vilevile chama hicho kinaitaka serikali iondoe Bungeni miswaada inayohusu vyama vya siasa na uchaguzi, ambayo ni muswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya siasa na Sheria ya gharama za Uchaguzi.
Katika Manndamano Hayo wakubwa kwa wadogo, wanawake kwa waume walijitikeza wakiwa na mabango na bendera ya chama hicho. pia walikuwa wakiimba nyimbo za kuisifu Chadema.
Baadhi ya wanawake wameibuka kwenye maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia ya Maendeleo(Chadema) wakiwa wamevaa viroba (magunia) vyenye ujumbe tofauti.
Wanawake hao wamejitokeza Kituo cha Mbezi Luis, Dar es Salaam leo Januari 24, 2024 ambako maandamano hayo yataanzia.
Wanawake hao wanaofanya biashara ya kuokota chupa, wamesema wamebuni vazi hilo wakilenga kufikisha ujumbe kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
“Tumevaa hivi kwa kuwa kitu ambacho ni rahisi kukipata kwa sasa ni kiroba, maisha yamekuwa juu na familia nyingi zinateseka tukiwamo sisi,” amesema mmoja wa wanawake hao.
Wamesema wao sio wanachama wala wafuasi wa Chadema, lakini wanashiriki maandamano hayo kama wananchi wa kawaida kutokana na kuvutiwa na ajenda za Chadema kwenye maandamano hayo.