Ukurasa wa YouTube wa Diamond Platnumz umerejea baada ya kudukuliwa, jambo ambalo lilisababisha kusimamishwa kwa akaunti hiyo.
Ukurasa huo una wafuasi zaidi ya milioni 6.5, ulisemekana kulidukuliwa siku ya Jumapili.
Afisa wa lebo ya Diamond Platnumz, Wasafi, alisema wamepokea barua pepe kutoka YouTube ikiwataarifu kuwa akaunti hiyo imesimamishwa.
Siku chache nyuma mkuu wa idara ya Digital wa Wasafi TV aliripoti kudukuliwa kwa Channel hiyo ambayo ilkuwa inaonesha maudhui yanayohusu maswala ya fedha za mtandanoni (Crypto currency) kinyume na maudhui yake ya kawaida.
Hii ni kawaida kwa mtandao wa Youtube kufungia Channel zilizoripotiwa kudukuliwa, Youtube huzifuta channel zilizoripotiwa kudukuliwa hadi wanafanye uhakiki wa mmiliki halali wa channel hiyo.
Majidi Ramadhani alisema chanel ilisitishwa baada ya wadukuzi hao kuweka wazi maudhui ambayo yalikiuka miongozo ya jukwaa la kidijitali,alisema kwamba wamepata hasara kubwa na wanajitahidi kusuluhisha suala hilo.
Siku ya Jumatatu, nyota huyo wa muziki aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akieleza kuwa ukurasa wake wa Youtube umerejea.
“Asante Mpenzi wangu….chaneli yangu ya Youtube imerejea,” alisema.