Search
Close this search box.
Africa

China kutoa dozi bilioni moja za chanjo ya UVIKO 19 kwa Afrika

11

Rais Xi Jinping wa China Jumatatu aliahidi kutoa dozi bilioni moja za chanjo ya UVIKO 19 kwa Afrika. Rais Jinping alisema hayo katika hotuba iliyotolewa kwa njia ya video kwenye mkutano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Diamniadio karibu na mji mkuu wa Senegal Dakar.

Ahadi ya Xi inakuja kama sehemu ya kongamano kati ya China na mataifa ya Afrika lenye msisitizo katika biashara na usalama, lililofanyika mjini Diamniadio.

Kulingana na ubalozi wa China mjini Dakar, China inawekeza zaidi barani Afrika kuliko mataifa mengine ya Ulaya na ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika na biashara ya moja kwa moja yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 200 katika mwaka 2019 pekee.

Viwango vya chanjo barani Afrika ni vya chini sana vikilinganishwa na mataifa mengine duniani, huku mataifa mengi yakijitahidi kugawa chanjo hizo ili kusaidia nchi za Afrika ambazo zinakabiliwa na changamoto za uzalishaji wa chanjo hizo kutokana na gharama kubwa ya kuzalisha chanjo.

Comments are closed

Related Posts