Dawa ya kupunguza uzani ya Novo Nordisk ya Wegovy sasa inapatikana kwa matumizi nchini China.
Kampuni ya Demark ilithibitisha kwa kituo cha Habari cha AFP siku ya Jumanne, huku taifa hilo la Asia likipambana na viwango vya juu vya unene wa kupindukia.
Kampuni ya dawa ya Denmark ndiyo waundaji wa matibabu mawili ya kubadilisha ugonjwa wa kisukari na unene uliokithiri — Ozempic na Wegovy — na kuendeleza kuibuka kwake kama kampuni ya thamani zaidi barani Ulaya.
Wegovy iliidhinishwa kutumika nchini Uchina mnamo Juni, na vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba agizo la kwanza katika hospitali ya umma lilitolewa huko Shanghai Jumatatu.
Msemaji wa Novo Nordisk alithibitisha kwa AFP siku ya Jumanne kwamba dawa hiyo “sasa inapatikana nchini Uchina” kwa matibabu ya watu wazima walio na unene uliokithiri na wale walio na uzito kupita kiasi na angalau ugonjwa mmoja unaohusiana na uzito.
Maendeleo ya haraka ya uchumi wa China yamechochea uboreshaji wa afya katika miongo ya hivi karibuni lakini ukuaji huo pia uliambatana na mlipuko wa matatizo yanayohusiana na uzito.
Kulingana na utafiti uliofanywa kupitia marika mwaka jana ambao uliandikwa na vyombo vya habari vya serikali , takriban nusu ya watu wazima wote nchini Uchina wana uzito mkubwa au wanene kupita kiasi,
Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuwa utoaji wa Wegovy kwa mwezi utagharimu karibu yuan 1,400 ($193), ikilinganishwa na bei iliyoripotiwa ya orodha ya Marekani ya dola $1,349.
Wiki iliyopita Novo Nordisk ilichapisha ongezeko la asilimia 21 la faida halisi hadi kroner bilioni 27.3 (ikiwa ni dola bilioni 3.94) katika robo ya tatu, licha ya vikwazo vya uzalishaji.
Kampuni hiyo ilisema ilitarajia mauzo ya mwaka mzima kupanda kwa asilimia 23 hadi 27 kutoka mwaka uliopita, kurekebisha utabiri wake wa awali wa asilimia 22 hadi 28.