ECOWAS yaiwekea Guinea vikwazo

Viongozi kutoka mataifa ya Afrika magharibi wanachama wa jumuiya ya ECOWAS wameagiza kufanyika kwa uchaguzi kufuatia mapinduzi ya serikali 5 Septemba. Viongozi hao kutoka mataifa 14 ya Afrika Magharibi walikutana katika mji mkuu wa Ghana, Accra Alhamisi 16 kuzungumzia mustakabali wa Guinea baada ya mapinduzi.

ECOWAS ilizuia akaunti za benki na kuwawekea marufuku ya usafiri wanachama wa junta na familia zao, ikitaka junta kufanya uchaguzi kwenye miezi sita na kumuachilia Rais Alpha Conde.

Rais Alpha Conde

Wawakilishi wa ECOWAS walitoa ripoti baada ya mkutano wao na kiongozi wa junta ambaye pia aliongoza mapinduzi hayo Mamady Doumbouya. Mapinduzi ya Guinea yamezua wasiwasi wa kuzuka kwa machafuko ya kisiasa katika eneo la magharibi mwa Afrika hususan baada ya mapinduzi ya Guinea na ya Mali mapema mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya nje wa Ghana aliyeongoza ujumbe wa ECOWAS amesema kuwa huenda wakawekea taifa la Guinea vikwazo. Rais wa ECOWAS Jean-Claude Kassi Brou amesema bila shaka kuwa ECOWAS imeiwekea Guinea vikwazo.

“Haina haja kusubiri kwa muda mrefu kabla Guinea irejee kwa utaratibu wa
demokrasia”
Rais wa ECOWAS Jean-Claude Kassi Brou.

Rais wa ECOWAS Jean-Claude Kassi Brou.