Fahamu Kaka ambao wanacheza kandanda ya kimataifa kutoka barani Afrika.

Samuel Eto’o

Bara la Afrika limejaaliwa kuwa na nyota wachezaji katika kandanda ambao wanafanya vyema katika soka ya kimataifa. Kuna wachezaji maarufu kama vile George Weah wa Liberia ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or, Samuel Eto’o kutoka Cameroon, El Hadj Diouf, John Obi Mikel, Fredric Kanoute, Asamoah Gyan, Kolo Toure ,Didier Drogba na Roger Milla.

Ila je unafahamu kuwa kuna ndugu ambao wanacheza soka katika mataifa tofauti barani Afrika na kimataifa barani Ulaya?

Francois Omam-Biyik na Andre Kana- Biyik

Ndugu wa Cameroon Francois Omam- Biyik na Andre Kana- Biyik wanafahamika zaidi kwa kuwa ndugu wa kwanza kutoka Afrika kucheza soka ya kimataifa. Walichezea timu ya taifa ya Indomitable Lions katika Kombe la Dunia mwaka wa 1990 nchini Italia.

Kolo, Yaya na Ibrahim Toure

Kolo, Yaya na Ibrahim Toure kutoka Ivory Coast wamechezea klabu tofauti Ulaya. Kolo Toure amechezea Manchester City na Arsenal, Kaka mdogo Yaya Toure alijiunga na Kolo katika timu ya Arsenal. Katika msimu wa 2010/2011 kaka hao waliisadia timu ya Manchester City kushinda kombe la FA. Kaka yao mdogo Ibrahim Toure alichezea timu ya Misri ya El Makasa na timu ya Ufaransa ya Nice kabla kuaga dunia mwaka wa 2014 kutokana na saratani.

Kolo na Yaya Toure

Kevin Prince na Jerome Boateng

Kevin Prince na Jerome Baoteng ni ndugu wa kambo kutoka Ghana. Mwaka wa 2010 katika Kombe la Dunia lililofanyika Afrika Kusini walishangaza dunia walipochezea mataifa mawili tofauti.  Kevin Prince Boateng alichezea taifa la Ghana na kakake Jerome akachezea nchi ya Ujerumani. Tarehe 23 Julai walivunja rekodi za dunia walipopatana uwanjani kila mmoja akichezea timu tofauti. Kaka yao mdogo George Boateng pia alicheza kandanda ingawaje kwa kipindi kifupi.

Kevin Prince Boateng na Jerome Boateng

Andre, Jordan na Rahim Ayew

Andre, Jordan na Rahim Ayew ni watoto wa bingwa wa kandanda kutoka Ghana Abedi Pele. Abedi Ayew alifahamika zaidi katika kandanda kama Abedi Pele na alikuwa kapteni wa timu ya taifa ya Ghana Black Stars. Pele alichezea timu tofauti za Ulaya ikiwemo Lille na marselle za Ufaransa.

Wanawe Abedi Pele, Andre Ayew na Jordan wamechezea timu za Ufaransa za Marseille, kwa sasa Jordan anachezea timu ya Crystal Palace ya Uingereza, Andre Ayew anachezea timu ya Qatar Al Sadd, na Rahim anachezea Europa Fc ya Gibraltar.

MacDonald Mariga, Victor Mugubi, Thomas na Sylvester Wanyama

Ndugu wanne kutoka Kenya,MacDonald Mariga, Victor Mugubi, Thomas na Sylvester Wanyama wanachezea timu ya taifa ya Kenya na kandanda ya kimataifa. Kaka hao ni kati ya ndugu kutoka Afrika ambao wamefanya vyema katika kandanda. Baba yao alichezea klabu ya AFC Leopards miaka ya 80 na 90.  MacDonald Mariga alikuwa mkenya wa kwanza kucheza soka ya kimataifa, kwa sasa anachezea klabu ya Real Oviedo. Victor Mugubi anachezea klabu ya CF Montreal. Thomas na Sylvester Wanyama wanachezea vlabu vya Kenya.

MacDonald Mariga na Victor Wanyama

Ndugu wengine kutoka Afrika wanaofanya vyema katika soka ya kimataifa ni Asamoah na Baffour Gyan kutoka Ghana. Asamoah Gyan anafahamika zaidi baada ya kuisadia timu yake ya taifa kufikia robo fainali ya  Kombe la Dunia mwaka wa 2010. Asamoah amechezea klabu za Sunderland ya Uingereza na Legon Cities. Kakake Baffour Gyan amechezea kalbu ya Dynamo Moscow na Al Nasr Benghazi.