Fahamu kuhusu adhabu ya kifo duniani na mtoto wa miaka 14 aliyehukumu kifo kwa umeme.

Oktoba 10 inaashiria Siku ya Ulimwengu Dhidi ya hukumu ya Kifo.

Mataifa 108 yamefutilia mbali hukumu ya kifo kwa makosa yote, mataifa mengine 55 bado yanatoa hukumu hiyo kwa makosa ya kawaida.

Oktoba 10 inaashiria Siku ya Ulimwengu Dhidi ya hukumu ya Kifo. Kaulimbiu ya mwaka huu imejikita katika kulinda afya na haki ya wanawake na wasichana kote duniani.

Kulingana na ripoti ya shirika la Amnesty International ya 2020 ya hukumu ya kifo,thuluthi tatu ya mataifa yote duniani yamefutilia mbali hukumu hiyo.

Kwa jumla mataifa 108 yameondoa kabisa hukumu hiyo ya kifo kwa makosa yote, huku mataifa 28 yakiwa hayajamhukumu mtu yeyote kifo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita na mataifa 55 bado yanatoa hukumu ya kifo kwa makosa ya kawaida.

Takriban watu 483 wamehukumiwa kifo mwaka 2020 ikiwa ni idadi ndogo ya watu kuhukumiwa katika kipindi cha muongo mmoja kulingana na ripoti ya Amnesty International.

Mataifa manne ya Iran imetoa adhabu ya kifo kwa watu 246, Misri 107, Saudia Arabia 27 na Iraq 45 ikiwa ni 88% ya hukumu zote za mwaka wa 2020.

Amnesty International imerekodi adhabu ya kifo iliyopewa wanawake 16 ambao walikuwa kati ya watu 483 walihukumiwa kifo mwaka 2020.

Aina tano za hukumu zilitumiwa kwenye adhabu ya kifo mwaka wa 2020, iliyotumiwa zaidi ni kunyongwa na kuuliwa kwa risasi, hukumu hiyo ilitumiwa kwenye mataifa 15. Nchini Marekani kudungwa sumu ilitumika pakubwa katika adhabu ya kifo majimbo mengine Amerika yakitumia umeme, gesi ya sumu, kunyongwa na kupigwa risasi. Saudia Arabia ikitumia zaidi adhabu ya kukata shingo kwenye hukumu.

Katika historia, watu wachanga zaidi kuwahi kuhukumiwa kifo nchini Marekani alikuwa mvulana wa umri wa miaka 14 kwa madai ya kumbaka msichana wa umri wa miaka 8 mnamo mwaka wa 1915. Mvulana mwingine aliyehukumiwa kifo kwa umeme ni George Stinney aliyekuwa na umri wa miaka 14. George alihukumiwa kifo kwa madai ya kuwaua watoto wawili wa umri wa miaka 7 na 11 mwaka wa 1944.

George Stinney

Ingawaje George alisisitiza hakutenda mauaji hayo aliuliwa kwa umeme, miaka kadhaa baadae hukumu hiyo ilibatilishwa.

Watu mashuhuri waliowahi kupewa adhabu ya kifo ni Che Guevara. Che Guevara alikuwa kiongozi wa mageuzi ya kisiasa nchini Cuba na aliuliwa kwa kupigwa risasi akiwa na umri wa miaka 39.

Barani Afrika Patrice Lumumba,aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza kuchaguliwa kwa sheria katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo alipewa adhabu ya kifo Januari 1961 kwa kupigwa risasi.

Patrice Lumumba, aliyekuwa waziri mkuu wa DR Congo

Watu wengine maarufu kupewa hukumu ya kifo ni Bennito Mussolini kutoka Italia na Sadam Hussein.