Fisi Wanaodaiwa Kufugwa Na Binadamu Wazua Kizaa Zaa Bariadi Wakiua Kondoo 21

Jumla ya kondoo 21 wanasadikiwa kuuawa na wanyama wakali aina ya fisi katika kijiji cha Mahina kata ya Somanda huku kondoo wengine tisa wakiwa hawajulikani walipo.

Tukio la kondoo hao kuuawa limetokea usiku wa kuamkia Aprili 2,2025 katika mtaa huo ambapo kondoo waliouawa wanatoka familia tofauti.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,Simon Simalenga amesema msako mkali wa kuwatafuta fisi hao unaanza mara moja huku akiwata wanaofuga fisi hao kujisalimisha.

“Tunawataka hao wanaofuga fisi kujisalimisha mara moja kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa,”Amesema Simalenga.

Na Mariam John