Georgia Yalazimika Kubadilisha Mswada Tata Iliyokuwa imepitisha

Bunge la Georgia kwa kauli moja limepiga kura ya kuutupilia mbali mswada tata iliyokuwa imeipitisha hapo awali.

Hii ni baada ya mswada huo kukumbana na pingamizi kali kutoka kwa wananchini pamoja na mashirika ya kimataifa.

Kwenye sheria  hiyo tata ambayo inafahamika kama ‘’Russian Law’’, wananchi wa Georgia wamesema huenda sheria hiyo ikazima uhuru wa wanahabari na kuzuia Georgia kuwa mwanachama wa muungano wa bara ulaya (EU).

Vile Vile sheria hiyo linaloungwa mkono na chama tawala cha Georgia, Dream Party, linasema shirika lolote  linalo pokea zaidi ya asilimia 20 ya msaada kutoka mataifa ya kigeni, yasajiliwe kama maajenti wa kimataifa la sivyo yatozwe faini ya juu zaidi

Uamuzi huo  ulizua gumzokali  mitandaoni na kusababisha maandamano katika jiji kuu  la Tbilisi. Maelfu ya waandamanaji walipiga kambi katika bunge la taifa hilo kuwashurutisha wabunge kuutupilia mbali msawada huo.

Bunge hilo siku ya ijumaa ilizidiwa na msukumo ya wananchi na kulazimikwa kuutupilia mbali mswada katika awamu ya pili ya upigaji kura

Wabunge wote 36 ambao katika awamu ya kwanza walikuwa wameipitisha, walilazimika kubali kauli yao.