Daktari wa tajriba ya miaka mingi kutoka kaunti ya Nakuru, Kenya amehukumiwa kwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwachoma sindano zenye sumu.Inasemekana kuwa daktari huyo, aliwachoma watoto wake wawili wenye umri wa miaka 3 na 5 na insulini siku ya Jumapili 19, kabla kujichoma dawa hiyo.
Mkuu wa polisi Beatrice Kiragori,amethibitisha kisa hicho. Inaripotiwa kuwa daktari huyo James Gakara, aliamua kujitoa uhai wake na watoto wake baada ya ugomvi na mke wake. Mume na mke walikuwa na ugomvi kuhusiana na uamuzi wa mke kutaka kuendeleza elimu yake nje ya nchi.
Maafisa wa polisi walifaulu kumnusuru James Gakara na kumpeleka hospitali ambapo anaendelea kupata matibabu akiwa chini ya ulinzi mkali. Miili ya watoto imepelekwa katika mochuari ya Manispaa ya Nakuru.