Idriss Deby Itno ashinda uchaguzi wa urais Chad

Kiongozi wa kijeshi nchini Chad Mahamat Idriss Deby Itno ndiye mshindi wa uchaguzi wa  urais uliofanyika wiki hii katika taifa hilo,hii ni kulingana na matokeo yaliofanyika awali na kutangazwa usiku wa kuamkia Ijumaa na tume inayosimamia uchuguzi nchini humo.

Dedy Itno amejizolea asilimia 61 za kura huku Succes Masra akijizolea asilimia 18.5, matokeo ambayo upinzani ukiongozwa na mgombea mwenza mkuu, Succes Masra wametofautiana na matokeo hayo.

Matokeo ya kura hizo yalitarajiwa kutolewa Mei 21 ila yakakujia wiki moja mapema. Hali ya usalama katika taifa hilo kwa sasa si salama, baada ya milio ya risasi kusikika katika eneo la N’djamena, pindi matokeo hayo kutangazwa.

Ikumbukwe kuwa kura za kumchagua rais katika taifa la Chad lilicheleweshwa kwa muda mrefu baada ya taifa hilo kuwa chini ya uongozi wa kijeshi.

Mwaka wa 2021, Debris Itno alichukua Madaraka kutoka kwa baba yake aliyekuwa madarakani kwa miongo mitatu, na ambaye aliuawa akiwa madarakani, katika mapambano na waasi.

Taarifa zinasema kuwa hamna uchaguzi wowote ambao umewahi kushuhudiwa tangu taifa la Chad kupata uhuru mwaka wa 1960 kutoka kwa Ufaransa.

Chad ni taifa lenye utajiri wa mafuta na lina idadi ya watu milioni 18.