Maafisa wa usalama nchini Iran wamemkamata mwanahabari aliyechapisha mahojiano ya babake Mahsa Amini, ambaye kifo chake kilizua maandamano dhidi ya utawala wa taifa hilo.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Hendaw lenye makao makuu nchini Norway limesema kuwa, Nazila Maroufian mwandishi wa habari wa mjini Tehran alikozaliwa Amini alizuiliwa kuanzia siku ya jumapili.
Maroufian alikamatwa katika nyumba ya mmoja wa jamaa zake huko Tehran na kuhamishiwa gereza la Evin katika mji mkuu.
Mwanahabari huyo ambaye anafanya kazi na shirika la Ruydad 24, alichapisha mahojiano na babaye Mahsa Amini, Amini Amjad katika mtandao wa habari wa Mostaghel tarehe 19 mwezi Oktoba.
“Sikuwa na nia ya kujiua wala sina ugonjwa wowote wa kimsingi” alizungumza mwanahabari huyo kwa uchungu alipokuwa akitoa sehemu ya nakala hiyo, akiashiria hatari zinazowakabili wanahabari nchini Iran wanaoandika habari hiyo.
Pia alisema kwamba alishindwa kuchapisha mahojiano hayo kwa siku kadhaa na kwamba familia yake ilitishiwa maisha.
Mtandao wa Mostaghel tayari imeshatoa mahojiano hayo japo nakala iliyohifadhiwa inaonyesha babake alipinga kuwa mwanawe alikuwa na magonjwa ya msingi.
Familia ya Amini inashikilia kwamba alipokea kipigo kibaya kutoka kwa maafisa wa usalama. Hata hivyo mamlaka ya Iran imepinga madai hayo lakini hasira kuhusu kifo Mahsa kilizua maandamana ya muda kutoka kwa raia.
Amjad Amini amesema aliambiwa na afisa wa afya kwamba anafaa kuandika ripoti ya mwisho. “Kile nafanya haikuhusu kwa lolote”
Kichwa cha mahojiano hayo kilikuwa “Babake Mahsa Amini: Wanadanganya!”
Wanahabari hao wawili kutoka Iran waliosaidia kufichua taarifa kuhusu Amini kwa dunia tayari wamekamatwa na wamezuiliwa kwa kipindi cha mwezi mmoja katika gereza ya Evin.
Niloufar Hamedi aliripotia gazeti la Shardh akiwa katika hospitali aliyolazwa Mahsa akiwa hali mahututi kwa siku tatu kabla ya kufariki. Kulingana na familia ya mwanahabari huyo, alitiwa mbaroni tarehe 20 Septemba.
Naye Elahe Mohammadi mwanahabari anayefanya kazi na gazeti la Ham Mihan, alikwenda Sagez kuripoti kuhusu mazishi ya Amini ambayo yaligeuka kuwa maandamano ya kwanza. Alikamatwa tarehe 29 Septemba.
Kulingana na kamati ya kuwatetea wanahabari yenye makao makuu mjini New York (CPJ), wanahabari 54 wamekamatwa katika oparesheni hiyo huku makumi wakithibitishwa kuachiliwa kwa dhamana.