Search
Close this search box.
Environment

Italia: Kasisi atozwa faini kwa kupiga kengela za kanisa ovyoo!

16

Kasisi mmoja nchini Italia ambaye wakazi wanadai kuwa amekuwa akipiga kengele za parokia yake zaidi ya mara 200 kwa siku ametozwa faini na kuamriwa kutopiga kengele hizo mara kwa mara.

Don Leonardo Guerri kutoka kanisa la Santa Maria a Coverciano huko Florence amekuwa akizozana kwa miaka minne na majirani, gazeti la Corriere Fiorentino liliripoti Ijumaa.

Wakazi wa eneo la mashariki mwa Florence wanasema kelele za kengele kila siku kati ya 8am na 9pm ambazo zimekuwa zikipigwa kwa miaka huwazuia kufanya kazi, kupumzika au kulala.

Wakati wa sikukuu kengele hizo hupigwa kila nusu saa.

Baada ya miaka minne ya malalamiko, mashauri ya kisheria na majaribio ya viwango vya uchafuzi wa kelele, wakala wa kikanda wa ulinzi wa mazingira (ARPAT) huko Tuscany waliamua kuchukua hatua, na kumtoza Guerri faini ya euro 2,000 ($2,225), gazeti hilo liliripoti.

Padre bado anaruhusiwa kupiga kengele, lakini tu kwa ajili ya Misa na ibada ya mwisho ya siku saa kumi na mbili jioni.

Alipowasiliana na AFP, padre huyo alikataa kutoa maoni yake.

Baada ya  kuongezeka kwa idadi ya kengele za kanisa zinazoigwa kote Tuscany, Askofu Mkuu wa Florence, Kardinali Giuseppe Betori, alituma agizo mnamo 2014 kwa dayosisi yake iliyolenga kudhibiti viwango vya kelele.

Aliwataka makasisi kuepuka kuwasumbua wakaazi wa eneo hilo wanaoishi karibu na makanisa.

Comments are closed

Related Posts