Donald Trump alinusurika kwa tundu la sindano katika jaribio la mauaji kwenye mkutano wa kisiasa Jumamosi. Shirika la upelelezi ya nchini Marekani (FBI) sasa inachunguza tukio hilo.
Kilivyotokea:
- Trump, akiwa amevaa shati jeupe, koti jeusi, na kofia nyekundu ya MAGA, alikuwa akizungumza dhidi ya uhamiaji haramu wakati risasi zilipoanza kurindima saa 12:08 jioni.
- Trump alishika sikio lake la kulia huku risasi nne zikifyatuliwa, ikifuatiwa na risasi ya tano na ya sita.
- Maajenti wa Secret Service walimzunguka Trump haraka huku akiinama nyuma ya mimbari.
- Risasi zaidi zilifyatuliwa, zikisababisha hofu kwa umati.
- Ndani ya sekunde 22, vikosi vya usalama vilipanda jukwaani na Trump aliinuliwa na maajenti.
- Trump aliwahakikishia umati yuko salama, akaongozwa kutoka jukwaani, akasindikizwa hadi kwenye gari la usalama.
Jibu la Trump:
- Trump alichapisha kwenye Truth Social saa 2:42 usiku, akisema alipigwa risasi na kuhisi risasi ikipenya sikio lake la kulia.
- Rais Joe Biden alifahamishwa na kulaani tukio hilo, akikatisha mapumziko yake ya ufukweni kurudi Washington.
Mshambuliaji Alitambulika:
- FBI ilimtambulisha mshambuliaji kama Thomas Matthew Crooks, kijana wa miaka 20 kutoka Bethel Park, Pennsylvania.
- Crooks, aliyesajiliwa kama Republican, aliwahi kuchangia dola 15 kwa kundi la wapiga kura wa mrengo wa kushoto.
- Mshambuliaji alipiga risasi kutoka juu na alidhibitiwa na maajenti.
Waathiriwa:
- Mshambuliaji na mshiriki mmoja waliuawa; watazamaji wawili walijeruhiwa vibaya.
- Mashuhuda waliripoti kumuona mtu aliyepigwa risasi kichwani na mwanamke mwingine aliyepigwa risasi mkononi.
Polisi wa eneo hilo walijibu ripoti za shughuli za kutiliwa shaka lakini hawajatoa maelezo zaidi.