Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, John Heche amekamatwa na Jeshi la Polisi asubuhi ya leo April 24,2025 ambapo amekamatwa akiwa pamoja na Chacha Heche Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara na Walinzi wawili.

CHADEMA pia imesema Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika amekamatwa na Jeshi la Polisi asubuhi hii maeneo ya Fire akielekea Makama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu.
Wengine waliokamatwa ni John Pambalu ambaye ni Mkurugenzi wa Mafunzo, Oganaizesheni na Uchaguzi, Twaha mwaipaya, Elizabeth Mambosho Katibu wa Chama Wilaya Ilala na Lucas Ngoto Mwenyekiti wa Chama kanda ya Serengeti.
CHADEMA imesema wengine waliokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi cha Kati ni Swabrati Malonge, Manase Mjema, Naomi Kitabi, Abel Kirubi Mwandishi wa East Africa na wawili waliotambulika kwa jina moja Harun na Jackob.