Search
Close this search box.
People
Naibu rais Rigathi Gachagua.

Uraibu na mienendo yake ya kutangamana na watu kutoka matabaka mbalimbali ulimfanya rais wa Kenya anayeondoka Uhuru Kenyatta kulengwa na waraibu wa kubuni memes nchini humo.

Kila sehemu ya maisha yake kuanzia mavazi na hotuba yake kwa hadhira uliwekwa kwenye mizani na mara kwa mara wakenya wengi kuishia kubuni memes za kuvunja mbavu.

Hali hii ilipelekea rais Kenyatta kufuta ukurusa wake wa twita kwa misingi kuwa hangeweza kuendelea kutazama jinsi alivyopondwa kwenye mtandao huo wa kijamii.

“Hata Twita niliondoka huko niliona hiyo kitu ni bure ni matusi tu. Unakaa hapo unasoma hulali. Afadhali nilale nipige story na mama, nilale niamke niende kufanya kazi.” Alisema rais mstaafu.

Lakini Uhuru anapoondoka katika afisi ya umma, wakenya walikuwa na kibarua ya kupata atakayeridhi kutoka kwake ila sasa mfalme  mwingine wa kutesa mitandaoni amejitokea na si mwingine ila ni naibu wa rais muheshimiwa Rigathi Gachagua maarufu kama Riggy G.

Riggy G amedhihirisha kuwa atatoshea kwenye viatu vya Uhuru Kenyata au hata kwa bora zaidi katika masuala haya ya memes na kuwazingua wakenya mitandaoni.

Gachagua amejizolea memes kadhaa ila ni muhimu kusema kuwa amechukua uongozi vyema hasa baada ya kujikanganya akila kiapo, jambo ambalo limewaacha wakenya na kumfanya kuzungumziwa sana katika mitandao wengi wakisema “alichoma” wakati akiapishwa.

Bwana Giggy G nusra akiapishe. Huyu bwan kwa hakika atatuonyesha mambo katika hizi “streets.” Msanii Eddie Butita alinena kwenye twita.

Vilevile wakati wa mjadala wa manaibu wa marais katika chuo kikuu cha Catholic kabla ya uchaguzi mkuu wa agosti, Gachagua alipasua anga ndani ya ukumbi huo na baadaye katika mitandao ya kijamii alipowaambia wafawidhi  “pardon”

Hata hivyo umaarufu wa Gachagua ulitokana na jinsi anavalia makoti makubwa wakenya wenyewe wakiyaita “Likoti” suala ambalo alikiri siku chache zilizopita na kusisitiza kuwa hakuwa na wakati wa kununua mavazi mapya wakati wa kampeini.

Kuanzia kwa masuti makubwa yaliomvaa, koti zisizo size yake na jinsi anavyozungumza Gachagua amewapa wakenya jambo la kuzungumzia kwenye mitandao ya kijamii kwani wamepata kasoro kwa lolote ambalo amefanya.

Alipoteuliwa na chama chake cha UDA kama mgombea mwenza wa rais Ruto, Gachagua alijitokeza akiwa amevalia suti isiyomtosha na wengi wakashanaa iwapo naibu huyo wa rais anashonewa nguo na fundi mmoja na rais wa Uganda Yoweri Kanguta Museveni.

Wengi hata wakijitolea kumsaidia kubadili muonekano wake.

“Najua sehemu ambayo tunawezapata shuti ambazo zitakuchukua vizuri uonekane kama rais William Ruto,” mmoja wa watumizi wa twita aliandika.

Comments are closed