Serikali ya Tanzania ipo katika mazungumzo na Kampuni ya Adani kwa ajili ya mradi wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 900 kwa ajili ya kujenga mradi kubwa za nyaya za umeme. Hii ni kwa mujibu wa afisa kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki
Kwa mujibu wa David Kafulila, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Tanzania, Adani Group imeelezea nia yake kwa serikali ya Afrika Mashariki. Tanzania pia ipo katika mazungumzo na kampuni ya Uingereza ya Gridworks Development Partners LLP kwa ajili ya mradi wa umeme wa dola milioni 300 chini ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.
Kampuni hiyo ya bilionea wa India Gautam Adani inapanua wigo wake katika Afrika Mashariki kwa uwekezaji nchini Tanzania na nchi jirani ya Kenya. Mwezi Mei, Tanzania iliipatia mkataba wa miaka 30 wa kuendesha kituo kikuu cha kontena katika bandari ya Dar es Salaam.
Nchini Kenya, Adani iko katika mazungumzo na kampuni ya kusambaza umeme nchini humo kwa makubaliano ya kujenga nyaya za umeme zenye thamani ya dola milioni 736. Pendekezo la kundi hilo la kuendesha uwanja wa ndege wa kitaifa wa jomo kenyata wa taifa hilo katika mji mkuu wa Nairobi, limezua pingamizi kali kutoka kwa umma na kufunguliwa mashtaka mahakamani