Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Kanda Za Ngono Za Mtumishi Wa Serikali Ya Equatorial Guinea Zazua Gumzo Mitandaoni - Mwanzo TV

Kanda Za Ngono Za Mtumishi Wa Serikali Ya Equatorial Guinea Zazua Gumzo Mitandaoni

Mamia ya kanda za ngono zinazomhusisha mtumishi wa serikali wa ngazi ya juu wa taifa la Equatorial Guinea pamoja na wake za wanaume tajika zimeenea kwenye mitandao ya kijamii, na kusababisha mamlaka kujaribu kuzuia kuenea kwa video hizo.

Kanda Za Ngono Za Mtumishi Wa Serikali Ya Equatorial Guinea Zazua Gumzo Mitandaoni

Katika video hizo ambazo zilisambaa katika mitandao ya WhatsApp, Tiktok, X  (Twitter), Instagram, Facebook, na kwingineko, mkurugenzi wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha (ANIF), Baltasar Ebang Engonga, anaonekana akiwa na wanawake mbalimbali – wakiwemo wake za maafisa mashuhuri -ofisini kwake katika wizara ya fedha.

Siku ya Jumatatu, makamu wa rais wa nchi hiyo Teodoro Nguema Obiang Mangue alitangaza kwenye X kwamba serikali itaamuru “kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi wote wa umma ambao wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi katika ofisi za wizara, kwani hii ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za maadili na sheria ya maadili ya umma”.

Si mara ya kwanza kwa kanda za ngono zinazohusisha watumishi wa umma kuvuja kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini suala hilo limevuma kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea kutokana na sifa mbaya za viongozi waliohusika.

Wiki iliyopita, Obiang alisema kuwa ametoa notisi ya saa 24 kwa wizara ya mawasiliano ya Guinea ya Ikweta, mdhibiti na makampuni ya simu “kuzuia usambazaji wa video za ngono ambazo zimejaa mitandao ya kijamii nchini Equatorial Guinea”.

“Kama serikali, hatuwezi kuendelea kuona familia zikiharibiwa,” makamu wa rais anayehusika na ulinzi na usalama alisema.

Kulingana na akaunti zilizosambazwa kwa mara ya kwanza na vikundi vya Whatsapp na kisha kuwekwa kwenye Facebook, Instagram, TikTok na X, Engonga alipiga zaidi ya video 400 za ngono ofisini kwake.

Kanda hizo za ngono zilivujishwa kwenye mitandao ya kijamii wakati ambapo alikuwa amewekwa rumande katika gereza maarufu la Black Beach la Malabo katika kesi ya ubadhirifu wa fedha za umma, kulingana na kituo cha televisheni cha serikali TVGE.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Equatorial Guinea Anatolio Nzang Nguema, aliihakikishia TVGE kwamba ikiwa uchunguzi wa kimatibabu utabaini kuwa Ebang Engonga “alikuwa na ugonjwa wa zinaa” atafunguliwa mashtaka kwa kosa dhidi ya “afya ya umma”.