Bondia maarufu wa Tanzania Karim ‘Mtu Kazi’ Mandonga amepigwa na Bondia Moses Golola wa Uganda kupitia ‘’Technical Knockout’’ katika roundi ya tatu ya pambano kali lililochezwa siku ya jumamosi usiku jijini Mwanza.
Pigano hilo la kukata na shoka lilivutia umati mkubwa wengi wakiwa ni mashabiki wa Mandonga aliyekuwa amewaahidi ushidi. Awli akihijiwa na wanahabari, Bondia Huyo alisema amemuandalia Golola Ngumi kali ijulikanyao kama Ndukube.
Ikumbukwe ndani ya siku nane, Mandonga amepigana mapambano mawili na amepoteza yote
Julai 22, Mandonga alipigwa na Bondia Daniel Wanyoni wa kenya .