Katibu Mkuu wa Umoja Wa Kimataifa Antonio Guterres Ahofia Hatari zaidi Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea wasiwasi mkubwa kutokana na hatari ya kuongezeka na kutanuka kwa mzozo huo, na ametahadharisha umuhimu wa kuwalinda raia.

Guterres amerejelea msimamo wake wa kulaani shambulio la Hamas la Oktoba 7 na kuamuru kuachiwa huru mateka wote, lakini akaalani pia mauaji ya raia huko Gaza na kusisitiza kuwa amesikitishwa na ripoti iliyobainisha kwamba theluthi mbili ya waliouawa huko Gaza ni wanawake na watoto. Hadi sasa, wizara ya afya imesema watu 8,525 wameuawa Gaza huku 3,500, miongoni mwa hao ni watoto.

United Nations Secretary General Antonio Guterres (C) visits the Maya Devi Temple at the UNESCO World Heritage Site of Lumbini on October 31, 2023, as part of his four-day visit to in Nepal. (Photo by PRAKASH MATHEMA / AFP)

jeshi la ulinzi la Israel IDF limeendeleza mashambulizi usiku wa kuamkia leo, mashambulizi yake katika maeneo mbalimbali ya Gaza na limethibitisha kuwa limefanya shambulio kwenye kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa ukanda huo.

Msemaji wa jeshi la Israel Luteni Kanali Richard Hecht ameliambia shirika la habari la Marekani CNN kwamba walimlenga kamanda mkuu wa Hamas aliyekuwa katika eneo hilo. Israel ambayo imekuwa ikifanya operesheni kadhaa za ardhini, imesema pia kuwa wanajeshi wake wawili wote wakiwa na umri wa miaka 20, wameuawa jana Jumanne huko Gaza huku wengine wawili wakijeruhiwa.

Wizara ya Afya inayodhibitiwa na kundi la Hamas imesema shambulio hilo kwenye kambi ya wakimbizi limesababisha vifo vya watu 50 na kuwajeruhi wengine karibu 150.