Search
Close this search box.
Africa

Kenya imefaulu kuwachanja wakenya milioni 14 katika zoezi la kuwachanja wakenya dhidi ya UVIKO-19.

Katika taarifa, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kuwa watu milioni 6.5 wamechanjwa kikamilifu.

Alisema kuwa dozi 372,136 zilitolewa kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 15 na 17.

“Katika saa 24 zilizopita jumla ya chanjo 197,231 zimetolewa. Jumla ya watu waliopatiwa chanjo kamili katika saa 24 zilizopita ni jumla ya watu 93,111 huku watu 104,120 wakipokea chanjo yao ya kwanza,” alisema.

Alisema kwamba “idadi ya watu wazima waliopatiwa chanjo kamili ni 24.0% na waliochukua dozi ya pili kati ya wale waliopata chanjo ya kwanza ni 63.3%.

Serikali inalenga kuwachanja watu 27,246,033.

Kaunti ya Nyeri inaongoza kwa idadi ya chanjo zilizotolewa huku watu wazima 228,456 wakiwa wamechanjwa kikamilifu.

Kwa watu wazima 337,296, ni watu 25,179 tu wamechanjwa ambayo ni 7.5% ya jumla ya watu wote.

Kaunti ya Nairobi ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya dozi za nyongeza zilizopokelewa (77,886) ikifuatwa na Nakuru (15,591) kisha Kiambu (12,916).

Wajir, Marsabit na Lamu wana idadi ndogo zaidi ya watu waliopokea nyongeza hiyo ikiwa ni watu 65,63 na 37 mtawalia.

Comments are closed