Kenya kuandaa kongamano la Afrika na Ufaransa mwaka 2026

Kenya inatarajiwa kuandaa kongamano la Afrika na Ufaransa mwaka 2026 kwa mara ya kwanza tangu lizinduliwe mwaka 1973.

Itakua mara ya kwanza kwa kongamano hilo kuandaliwa nje ya mataifa yanayozungumza Kifaransa au Ufaransa.

Haya yamefikiwa Ijumaa baada ya Marais William Ruto wa Kenya na Emmanuel Macron wa Ufaransa kukutana pembezoni mwa mkutano wa 79 wa Umoja wa mataifa mjini New York Marekani.

Kongamano hilo litawaleta pamoja viongozi ,Marais,sekta za kibinafsi na makundi ya kijamii.

Itakuwa mara ya kwanza baada ya miaka 53 kwa kongamano hilo kuandaliwa na taifa linalozungumza Kiingereza.