Search
Close this search box.
East Africa

Kenya: Mahakama yasimamisha matumizi ya sajili iliyochapishwa

19
Mahakama ya rufaa imesimamisha utumizi wa sajili iliyochapishwa.

Mahakama ya rufaa imesimamisha uamuzi iliyotolewa na Mahakama kuu ikiagiza Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi (IEBC) kutumia sajili iliyochapishwa .

Mahakama hiyo ya rufaa imesema” Chama cha United Democratic Alliance (UDA) Iimefaulu kuonyesha haja ya kuidhinisha uamuzi uliotolewa tarehe 4 mwezi agosti mwaka wa 2022 katika mahakama kuu ya Nairobi katika kesi ya katika  nambari E306 ya 2022 ikisubiri kusikizwa na kuamuliwa na rufaa hiyo.

Uamuzi huo unatokea baada ya chama cha UDA kuwasilisha kesi kupitia wakili Elias Mutuma ukipinga uamuzi uliotolewa wiki iliyopita .

Mutuma alisema uhalali wa uchaguzi mkuu unaweza kuathiriwa na matumizi mabaya ya sajili iliyochapishwa kwa kuwa sajili hiyo haina njia ya kuhakikisha hakuna udanganyifu.

Chama cha UDA kimesema kuna uwezekano wa kutokea mkanganyiko katika utekelezaji wa sheria inayoshughulikia njia ya kuwatambua wapiga kura wakati wa uchaguzi.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema watafuata uamuzi wa kutumia sajili ya kielektroniki kama njia ya msingi ya kuwatambua wapigakura.

“Tume itazingatia uamuzi wa mahakama na tayari tumeagiza maafisa wa IEBC ambao tumewapa mafunzo ya kutosha kufuata maagizo yaliotolewa na mahakama,” Amesema mwenyekiti huyo.

Chebukati amesisitiza kuwa sajili ya kielektroniki ni sawa na iliyochapishwa.

Comments are closed

Related Posts