Mfanyabiashara Stanley Livondo mnamo Jumatatu, Februari 21, alisisitiza madai ya kuwepo kwa njama ya mauaji dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta.
Livondo alizungumza na waandishi wa habari baada ya kuandika taarifa na Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), akidai kuwa baadhi ya mamluki walioajiriwa kufanya kazi hiyo ya mauaji wako tayari kusaidia vyombo vya dola katika uchunguzi wao.
Aliongeza kuwa amekipatia chombo cha uchunguzi maelezo ya watu anaoamini kuwa ni sehemu ya kundi hilo ikiwa ni pamoja na majina yao, namba za usajili wa magari wanayotumia na jinsi yanavyofanya kazi.
Pia alidai kuwa mpango huo ulihusisha watu kutoka mataifa ya nje.
“Nimewapa (DCI) taarifa zote ikiwa ni pamoja na namba za magari wanayotumia, mahali wanapojificha,sehemu wanapotembea na kuwasiliana na jinsi wanavyotekeleza mipango yao,” alisema.
Livondo alibainisha kuwa taarifa alizotoa zitasaidia maafisa wa DCI kuchunguza na kuanza kuwavua watu hao kutoka mafichoni mwao siku zijazo.
“Tishio hilo litaondolewa saa yoyote kuanzia leo. Watachukuliwa mmoja baada ya mwingine, ikiwa ni pamoja na wale ambao wamejaribu kuwatishia au kuwaua mashahidi. Ni jambo kubwa ambalo linahusisha hata kanisa,” alitangaza.
Mfanyabiashara huyo alitoa maoni yake kuwa baadhi ya watu na mashahidi walikuwa tayari kutoa ushahidi wao, ilimradi serikali iwawekee ulinzi.
Huku akipuuza hofu yoyote kwa maisha yake, pia alikanusha kuwa madai yake yamechochewa kisiasa, akisema kwamba alikuwa na wasiwasi tu na Mkuu wa Nchi.
“Sigombei kiti chochote, lakini ni haki yangu kama Mkenya mzalendo kutoa ripoti kuhusiana na vitisho vyovyote kwa usalama wa Rais. Hilo ni jukumu langu kama raia. Kuhusu wakati, itabainika lini. vyombo vinaanza kuwakamata watu hawa” alibainisha.
Aliongeza kuwa atarekodi taarifa ya pili baadaye wiki hii siku ya Alhamisi.
DCI ilikuwa imemwita Livondo kuhusu matamshi yake aliyotoa Februari 19 wakati wa hafla ya Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria, ambapo alidai kuwa kumekuwa na majaribio mawili tofauti ya kutaka kumuua Rais Kenyatta.
Mawakili wa Stanley Livondo aliyewahi kugombea kita cha ubunge katika eneo bunge la Lang’ata walibaini kuwa mfanyabiashara huyo hakuwa na kesi ya kujibu na kwamba aliitwa tu kutoa ushahidi.
Matamshi yake yalizua taharuki katika ya wananchi na wanasiasa wa marengo tofauti.
“Kama mratibu wa mkutano wa maombi ya shukrani huko, huenda nisiwajibike kwa yale wasemaji walisema, lakini ulikuwa mkutano wangu, na lazima niwajibike. Leo nimemwomba mkuu wa DCI George Kinoti kumkamata Stanley Livondo kufuatia matamshi yake.” Mwanasiasa Moses Kuria aliandika katika barua yake kwa DCI.