Kenya na Zimbabwe zimeondolewa kwenye mechi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 kwa kuwa “zimeshindwa kujiondoa kwa vikwazo walivyowekewa na FIFA,” Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) lilisema Jumanne.
FIFA ilikuwa imesimamisha mashirikisho yote mawili mnamo Februari 24 kutokana na ‘uingiliaji wa serikali.’
“Kutokana na kushindwa kuoundoa vikwazo vilivyowekwa na FIFA, CAF imethibitisha kuwa Kenya na Zimbabwe hazitashiriki mechi za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cote d’Ivoire 2023,” ilisoma taarifa ya CAF.
“Michuano ya kufuzu itaanza siku ya kwanza ya Juni 2022.”
“CAF ilikuwa imewajumuisha katika droo rasmi mapema Aprili 2022 kwa masharti kwamba adhabu hiyo lazima iondolewe wiki mbili kabla ya siku yao ya kwanza ya mechi.”
Kenya walikuwa wamejumuishwa kwenye Kundi C pamoja na Burundi, Cameroon na Namibia huku Zimbabwe wakiwa Kundi K pamoja na Liberia, Morocco na Afrika Kusini.
Washindi na washindi wa pili katika makundi 12 wanafuzu kwa fainali katika vituo sita nchini Ivory Coast kwa tarehe zitakazotangazwa Juni na Julai mwaka ujao.
Mabingwa Senegal watatetea ubingwa wao wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) wakiwa nyumbani dhidi ya Benin.