Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Kenya: Tukio la ajabu twiga pacha wazaliwa - Mwanzo TV

Kenya: Tukio la ajabu twiga pacha wazaliwa

Mapacha adimu wamezaliwa na twiga aina ya Maasai katika mbuga ya wanyama ya Nairobi, Waziri wa wanyamapori wa Kenya alisema Jumanne.

“Hili ni tukio nadra sana,” Najib Balala alisema kwenye Twitter katika chapisho lililoambatana na picha ya mama huyo akiwaangalia pacha hao.

Spishi refu zaidi duniani ya Maasai iliorodheshwa kuwa “inayoweza kukabiliwa na kutoweka” kwenye Orodha Nyekundu ya Wanyama waliohatarini kutoweka ya 2016.

Kuna takriban twiga 117,000 pekee waliosalia porini, kulingana na Wakfu wa Uhifadhi wa Twiga.

Ilisema idadi ya wanyama hao barani Afrika imepungua kwa asilimia 30 katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, likieleza kuwa wanyama hao wamekuwa wakitoweka taratibu kwa miaka mingi.

Kenya ni nyumbani kwa spishi tatu ndogo za twiga, Maasai, reticutated na Rothschild.

Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi iko kilomita saba tu kutoka katikati mwa mji mkuu wa Kenya, na ni kivutio cha watalii kutokana na wanyamapori wake wakiwemo simba, chui, vifaru na Nyati.

Twiga huwa na mojawapo ya vipindi virefu zaidi vya mimba kwa mamalia ikiwa ni miezi 15.

Twiga huzaa wakiwa wamesimama, ambayo ina maana kwamba ndama wao huanguka chini urefu wa karibu mita mbili.

Kuanguka huko huwafanya wasimame na kukimbia chini ya saa moja baada ya kuzaliwa.

Ndama aliyezaliwa ni mkubwa kuliko mtu mzima wa kawaida.

Ni ndama wachache tu waliozaliwa mapacha ambao wamerekodiwa ulimwenguni kote na mara nyingi hufariki baada ya kuzaliwa.

Twiga wanaoishi porini wanaweza kuishi kwa hadi miaka 25, na wale waliokatika mbuga kizuizi huishi kwa hadi miaka 35.