Search
Close this search box.
East Africa

Uhaba mkubwa wa kondomu umekumba mji wa Naivasha huku mashabiki wa mashindano ya magari wakiendelea kumiminika kwenye sehemu maarufu ya mapumziko ili kutazama michuano ya Dunia ya Safari Rally yanayoendelea.

Mashindano hayo yalianza Alhamisi na yatahitimishwa Jumapili, Juni 26. Jiji la Naivasha limeshuhudia ongezeko la wageni, wakiwemo wafanyabiashara wa ngono na kusababisha uhaba wa kondomu.

Naivasha, inajulikana zaidi kwa wapenda burudani kama Vasha, ni sehemu maarufu kwa wapenda likizo.

Stanley Ngara, anayejulikana kama “Mfalme wa Kondomu” anasema kondomu za serikali ya Kenya zinazosambazwa kwa bure zimeisha.

“Tumeweza kununua na kusambaza kwa Wakenya.

Mahitaji ni makubwa sana hata tunapozungumza.

“Wafanyabiashara ya ngono wana shughuli nyingi,” Stanley alisema.

Mfalme wa Kondomu hutumia siku zake kuelimisha watu kuhusu mbinu salama za ngono na kusambaza kondomu.

Ana shauku kubwa ya kuongeza uelewa juu ya masuala ya afya ya uzazi na haki za ngono, ikiwa ni pamoja na VVU na UKIMWI.

Stanley anasambaza kondomu bure kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana, wafanyabiashara ya ngono, waendesha bodaboda, wanafunzi wa vyuo vikuu, wafanyabiashara sokoni na hata watumiaji wa dawa za kulevya.

Anasema amekuwa mtu mwenye shughuli nyingi tangu hafla ya Safari Rally ilipoanza Alhamisi.

“Biashara nyingi sasa zinafanya kazi kwa masaa 24.

“Nimezungumza na mfanyabiashara wa hoteli na anasema mauzo yake ya kondomu yameongezeka

Alisema tangu kondomu za bure kutoka kwa serikali kuisha, wamelazimika kununua kati ya 7,000, hadi 10,000 kwa msaada wa AIDS Healthcare Foundation (AHF), shirika la UKIMWI duniani ili kusambaza kwa makundi yaliyo hatarini zaidi – wafanyabiashara wa ngono.

“Kama ilivyokuwa Alhamisi usiki tulifanya ukaguzi na hakukuwa na mfanyikazi wa ngono mitaani na ni wengi sana hiyo inamaanisha kuwa shughuli nyingi zinafanyika hapa Naivasha,” Stanley alisema.

Hata hivyo, alikuwa mwepesi kusema kwamba uhaba wa kondomu umeikumba nchi nzima.

Ripoti ya 2019 kuhusu hali ya sasa ya VVU nchini Kenya ilifichua kuwa ni asilimia 44 pekee ya wanaume waliripoti kutumia kondomu wakati wa kujamiiana.

Ilisema ni kondomu 14 pekee zinazotumiwa na mwanamume mmoja kwa mwaka dhidi ya lengo la kimataifa la kondomu 40 kwa kila mwanaume kwa mwaka.

Asilimia 40 pekee ya wanawake waliripoti kutumia kondomu mara ya mwisho wa kujamiiana na wapo hatarini zaidi.

Comments are closed