Search
Close this search box.
Kenya

Kenya: Watu 33 wafariki baada ya basi kutumbukia mtoni

18

Watu 33 waliuawa wakati basi walilokuwa wameabiri kutumbukia mtoni katika eneo la Kati mwa Kenya afisa wa eneo hilo alisema Jumatatu.

Ajali hiyo ilitokea Jumapili jioni wakati basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Meru kuelekea Mombasa.

Basi hilo lilitumbukia kwenye daraja karibu mita 40 kwenye bonde la mto Nithi.

Picha zilionyesha basi hilo likiwa limepasuka baada ya kubingirika kwenye mteremko mkali, huku ripoti zikisema mabaki na miili ilikuwa imetapakaa majini na kwenye ukingo wa mto.

Watu 20 walifariki papo hapo siku ya Jumapili, huku wanne wakifia hospitalini na miili mingine sita kupatikana Jumatatu, kamishna wa kaunti Norbert Komora alisema.

“Msako bado unaendelea na tunajaribu kupata mabaki ya basi,”alisema.

“Uchunguzi bado unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo iliyotokea eneo la Nithi.”

Comments are closed

Related Posts