Search
Close this search box.
Africa
Malkia Strikers

Kenya imejishindia tiketi ya kushiriki mashindano ya FIVB World Championship baada ya kufika fainali ya mashindano ya voliboli ya wanawake ya bara Afrika mjini Kigali, Rwanda.

Timu ya Cameroon, ilishinda mashindano ya voliboli ya wanawake Afrika baada ya kuichabanga timu ya Kenya kwa 3-1 kwa seti za (25-21, 25-23, 15-25, 25-23) katika fainali ya michezo hiyo. Malkia Strikers ya Kenya na timu ya Cameroon zimefuzu kuwakilisha Afrika katika mashindano yajayo ya FIVB Women’s World Championship. Mashindano hayo yatafanyika Poland na Uholanzi 2022.

Timu ya Morocco iliibuka ya tatu baada ya kuichabanga Nigeria 3-0 kwa seti za (25-19, 25-17, 25-18) na kujishindia medali yake ya kwanza tangu mwaka 1987 waliposhinda medali ya fedha.Tunisia ilikuwa ya 5 baada ya kuishinda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa 3-0 kwa seti za (25-17, 25-11, 25-20).

Comments are closed