Mshukiwa wa mauaji nchini kenya Kevin Kang’ethe amesafirishwa kutoka Kenya hadi Marekani kujibu mashtaka ya kumuua mpenzi wake Margaret Mbitu.
Kupitia idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga, Kang’ethe alifaulu kurejeshwa Jumapili na atakabiliwa na kesi mjini Boston Jumanne, Septemba 3.Katika taarifa yake kwa vyomba vya habari, DPP Ingonga alithibitisha dhamira yake ya kuunga mkono Marekani, hasa timu ya waendesha mashtaka wanapoendelea na awamu inayofuata ya kesi hiyo.
Hapo awali Ingonga alikuwa amemhakikishia Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray mnamo Juni 2024 kwamba ofisi yake ina nia ya kuhakikisha haki inatendeka.Kang’ethe anasakwa nchini Marekani kwa mauaji ya Mbitu, mwenye umri wa miaka 31 ambaye mwili wake uligunduliwa ndani ya gari katika uwanja wa ndege wa Boston Logan mnamo Novemba 2023. Mwathiriwa aliripotiwa kuwa mpenzi wake.
Kisha mshukiwa alikimbilia Kenya na kujificha hadi alipokamatwa na mamlaka ya Kenya.
Baada ya kukamatwa mwezi Januari na kupewa agizo la kuzuiliwa kwa siku 30 ili kuruhusu mamlaka kufanya uchunguzi zaidi, Kang’ethe alitoroka kwa njia ya kutatanishakutoka kwa Kituo cha Polisi cha Muthaiga.