Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Kenya yatoa motisha ya kodi ili kuwavutia wawekezaji - Mwanzo TV

Kenya yatoa motisha ya kodi ili kuwavutia wawekezaji

Kenya imetoa motisha ya kodi ili kuwavutia wawekezaji wanaotaka kujenga viwanda vya kuzalisha chanjo za binadamu ikiwa ni pamoja na ya UVIKO -19.

Wawekezaji walio na uwekezaji wa angalau KSh10 bilioni watafurahia ushuru wa mashirika na mapato kwa viwango vya kipekee utakao jadiliwa na serikali kulingana na mabadiliko ya sheria kupitia Sheria ya Fedha, 2022 ambayo Rais Uhuru Kenyatta alitia saini kuwa sheria Ijumaa iliyopita.

Bunge lilifanyia marekebisho Sheria ya Ushuru wa Mapato, kupitia Mswada wa Fedha wa 2022, ili kutoa motisha ya ushuru kwa makampuni ambayo yatafanya uzalishaji wa chanjo nchini.

 â€œKampuni inayojishughulisha na biashara chini ya utaratibu maalum wa uendeshaji na serikali, iliyojumuishwa kwa madhumuni ya kutengeneza chanjo ya binadamu, ambayo uwekezaji wake wa mtaji ni angalau KSh10 bilioni, itatozwa kiwango cha kodi kilichoainishwa katika mpangilio maalum wa mfumo wa uendeshaji na serikali,” Sheria ya Fedha, 2022 inasema.

Kenya inatafuta kuanzisha kituo kamili cha uzalishaji wa antijeni kwa wingi chenye uwezo wa kuzalisha aina tofauti za chanjo. Bunge pia lilirekebisha Sheria ili kusamehe kodi kwa riba inayoonekana kuhusiana na mkopo usio na riba unaotolewa kwa kampuni inayozalisha chanjo za binadamu.

Gawio linalolipwa na kampuni inayojitolea kuzalisha chanjo za binadamu kwa mtu yeyote ambaye si mkazi na pia mapato ya kampuni inayotaka kutengeneza chanjo za binadamu chanjo hizo hazitatozwa ushuru wa mapato.

Mnamo Januari Kenya ilialika makampuni kupitia zabuni ya kimataifa kutoa zabuni ya ujenzi wa kiwanda cha chanjo ya Covid-19 cha Taasisi ya Kenya BioVax, kampuni ya kibiashara na utengenezaji inayomilikiwa na Serikali.

Serikali tangu wakati huo imechagua kampuni ya Kimarekani ya teknolojia ya Moderna kuanzisha kituo cha uzalishaji wa chanjo nchini Kenya, cha kwanza barani Afrika, kuzalisha chanjo ya messenger RNA (mRNA).

Rais Kenyatta alitangaza kwamba Kenya imeshirikiana na Moderna katika uanzishwaji wa kituo hiki cha utengenezaji wa mRNA kusaidia kuandaa nchi na mataifa mengine katika bara hili kupitia Umoja wa Afrika kukabiliana na majanga ya kiafya ya siku zijazo.

Mtendaji mkuu wa Moderna Stéphane Bancel alitangaza kwamba anatarajia kuwekeza takriban dola milioni 500 (KSh56.5 bilioni) kwa kiwanda hicho na kutoa dozi milioni 500 za chanjo ya mRNA kwa bara la Afrika kila mwaka.

Pia ina mpango wa kuanza kuongeza dozi za chanjo yake ya UVIKO-19 barani Afrika mapema kama 2023, kufuatia makubaliano na serikali ya Kenya.